Tunaamini afya bora hujengwa pia kupitia elimu na mawasiliano sahihi. Kupitia video, makala na mazungumzo ya ana kwa ana tunatoa elimu kuhusu afya ya uzazi, mfumo wa mkojo, lishe na ustawi wa mwili.
Ufuatiliaji wa mteja
Kila mteja anayepata huduma zetu hupokea mwongozo wa matumizi na hatua zinazofuata. Tunaendelea kuwasiliana naye kufuatilia maendeleo, kujibu maswali na kurekebisha ushauri kadri inavyohitajika. Mrejesho wa wateja hutusaidia kuboresha huduma zetu kila siku.
Tembelea sehemu ya Elimu ya Afya kutazama video na makala zetu.
Tahadhari: Taarifa zilizo kwenye tovuti hii ni za kielimu na hazichukui nafasi ya uchunguzi wa kitabibu, ushauri wa mtaalamu wa afya au huduma ya dharura. Kwa dalili kali au za dharura, tafadhali fika hospitali mara moja. Usiache dawa ulizoandikiwa bila ushauri wa mtaalamu wa afya aliyehitimu.